Hadithi

  • Imam Hassan Al-Mujtaba (a.s) anazo fadhila nyingi na daraja ya juu

    Sheikh Rajab Shaaban:

    Imam Hassan Al-Mujtaba (a.s) anazo fadhila nyingi na daraja ya juu

    Tunayo mengi ya kujifunza kutoka ndani ya Qur’an Tukufu na kutoka kwa Itrah wa Mtume, Ahlul-Bayt wake Watoharifu (amani iwe juu yao), ambavyo ndio vizito vyetu viwili na viongozi wetu baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w). Na kumsoma na kumzungumzia Imam Hassan Al-Mujtaba (s.a), na kujifunza mengi kutoka kwake juu ya Uislamu wetu na Maisha yetu, ni sehemu ya kushikamana kisawa sawa na Ahlul-Bayt (a.s), ambao ndio kizito cha pili kwa ukubwa baada ya Qur’an Tukufu.