21 Aprili 2025 - 17:12
Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na hatua za mashindano ya Qur'an Tukufu na Hadithi - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania,  2025

Tangazo la Matokeo ya mwisho litatolewa kuanzia Tarehe 01 - 05 - 2025 mpaka tarehe 05 - 05 - 2025. Na ratiba ya hafla ya fainali ya mashindano haya pamoja na ugawaji wa zawadi kwa washindi na washiriki utakuwa tarehe 17 - 05 - 2025 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere - Jijini Dar-es-Salam - Tanzania. 

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Hojjat Al-Islam wal Muslimin, Dar. Ali Taqavi, Mkuu wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania, akiendelea kufuatilia kwa karibu zaidi Mashindano ya 30 ya Qur'an Tukufu na Hadithi katika Hawzah ya Mabanati ya Hadhrat Zainab (s.a) iliyopo chini ya Jamiat Al-Mustafa (s), katika maeneo ya Kigamboni, Dar - ES - Salam, Tanzania. Mashindano haya ya Qur'an Tukufu yanajiri nchini Tanzania, Zanzibar na Burundi kwa kuwashirikisha Wanafunzi wa kike na kiume kutoka katika Hawza na Madarisi mbalimbali. Hivi sasa Mashindano haya yamefika nusru Fainali na yanaelekea Fainali.

Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na hatua za mashindano ya Qur'an Tukufu na Hadithi - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania,  2025

Mashindano haya ya Qur'an Tukufu yanaendeshwa kupitia hatua mbili muhimu: Hatua ya kwanza ya Mashindano haya ilikuwa ni hatua ya Mtihani wa Shafahi (Kuzungumza) uliofanyika tarehe 12 - 04 - 2025. Na Hatua ya mtihani wa Shafahi ilifanyika Siku ya Jumamosi tarehe 19 - 04 - 2025 saa 2 : 00 Baada ya Dhuhraini.

Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na hatua za mashindano ya Qur'an Tukufu na Hadithi - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania,  2025

Hatua ya pili ilihusiana na Mtihani wa Kat'bi (Kuandika), ambao ulikuwa na hatua moja tu, ambapo ulifanyika tarehe 19 , 04, 2025 Siku ya Jumamosi baada ya Adhuhuri.

Tangazo la Matokeo ya mwisho litatolewa kuanzia Tarehe 01 - 05 - 2025 mpaka tarehe 05 - 05 - 2025. Na ratiba ya hafla ya fainali ya mashindano haya pamoja na ugawaji wa zawadi kwa washindi na washiriki utakuwa tarehe 17 - 05 - 2025 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere - Jijini Dar-es-Salam - Tanzania. 

Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na hatua za mashindano ya Qur'an Tukufu na Hadithi - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania,  2025

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha