Tangazo la Matokeo ya mwisho litatolewa kuanzia Tarehe 01 - 05 - 2025 mpaka tarehe 05 - 05 - 2025. Na ratiba ya hafla ya fainali ya mashindano haya pamoja na ugawaji wa zawadi kwa washindi na washiriki utakuwa tarehe 17 - 05 - 2025 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere - Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.
Muislamu mwenye kuhifadhi Qur'an Tukufu na mwenye Elimu juu ya Qur'an Tukufu, huyo atakuwa ni mwenye kuangaziwa na Nuru ya Qur'an kaburini mwake, na Mtume Muhammad (s.a.w.w) atakuwa Shahidi wake kesho Siku ya Kiyama.