Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kibaha, Pwani - 31 Agosti 2025 - Mashindano ya 4 ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu yanaendelea kwa mafanikio makubwa yakiwa Mubashara kutoka Kibaha, Pwani yakihudhuriwa na waumini, viongozi wa dini, na wadau mbalimbali wa Qur’an kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mgeni rasmi katika hafla hii muhimu ni Samahat Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), ambaye tayari amewasili akiwa na kuongoza sehemu ya hotuba na mawaidha ya kiroho yenye kugusa nyoyo.
Katika hafla hiyo, washiriki mbalimbali -hasa vijana-wanaendelea kuonesha uwezo wao mkubwa wa kuhifadhi na kusoma Qur’an Tukufu kwa ufasaha, nidhamu na tajwidi ya hali ya juu.
Kauli mbiu ya mashindano haya ni:
“Hakika Qur’an ni Muongozo,” ikisisitiza nafasi ya Qur’an katika kuleta maadili, amani, na maendeleo ya kiroho katika jamii.
Tafadhali endelea kufuatilia matangazo haya mubashara kupitia mitandao ya kijamii, redio na televisheni zinazorusha tukio hili muhimu la kiroho.
Your Comment