Licha ya mshangao wa Waziri Mkuu Meloni kutokana na umbo na urefu wa mgeni wake, wapigapicha nao walijikuta katika wakati mgumu, huku baadhi yao wakilazimika kulala chini ili kuwakamata viongozi hao wawili katika fremu moja ya picha.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Italia na duniani kote baada ya kuonekana kuustajabia urefu wa Rais Daniel Chapo wa Msumbiji.
Tukio hilo lilijiri wakati Rais Chapo alipokuwa katika ziara rasmi nchini Italia, alipokewa na mwenyeji wake mjini Rome. Tofauti kubwa ya kimo kati ya viongozi hao wawili iliwavutia wengi, kiasi cha kuwa mada ya mjadala mpana mitandaoni.
Licha ya mshangao wa Waziri Mkuu Meloni kutokana na umbo na urefu wa mgeni wake, wapigapicha nao walijikuta katika wakati mgumu, huku baadhi yao wakilazimika kulala chini ili kuwakamata viongozi hao wawili katika fremu moja ya picha.
Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Mkuu Meloni ana urefu wa futi 5 na inchi 2 (5’2) huku Rais Chapo akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 8 (6’8), tofauti iliyoonekana wazi katika picha na video zilizosambaa kwa kasi mitandaoni.

Mitandao ya kijamii imelipuka kwa utani, memes na vikorombwezo, vikilenga zaidi tofauti ya urefu na maumbo ya viongozi hao. Baadhi ya watumiaji wamefikia hatua ya kumpa Meloni lakabu ya “MINI MELONI”, jambo lililozidisha mjadala na vichekesho katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali.
Your Comment