Maadhimisho hayo yalionesha urithi mkubwa na wa kina wa Sayyida Fatima Zahra (a.s) katika Uislamu, pamoja na umuhimu wake wa kudumu kama kielelezo bora katika maisha ya kidini ya kizazi cha sasa. Siku hii pia huadhimishwa kama Siku ya Mama, kuwakumbuka na kuwaheshimu akina mama, mabibi, dada na wanawake kwa ujumla.

17 Desemba 2025 - 14:16

Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Iran Nairobi Laadhimisha Maulid ya Sayyidat Fatima Zahra (s.a), Siku ya Mama na Heshima ya Mwanamke +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya liliadhimisha kwa furaha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Sayyida Fatima Zahra (a.s), binti mpendwa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika viwanja vya Kituo cha Utamaduni cha Iran jijini Nairobi.

Maadhimisho hayo yalionesha urithi mkubwa na wa kina wa Sayyida Fatima Zahra (a.s) katika Uislamu, pamoja na umuhimu wake wa kudumu kama kielelezo bora katika maisha ya kidini ya kizazi cha sasa. Siku hii pia huadhimishwa kama Siku ya Mama, kuwakumbuka na kuwaheshimu akina mama, mabibi, dada na wanawake kwa ujumla.

Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Iran Nairobi Laadhimisha Maulid ya Sayyidat Fatima Zahra (s.a), Siku ya Mama na Heshima ya Mwanamke +Picha

Hafla hiyo ilijumuisha usomaji wa Qur’ani Tukufu, mijadala ya kina ya tafakuri, pamoja na mashairi yenye hisia, yote yakilenga kuadhimisha hadhi ya kipekee na isiyo na mfano ya Sayyida Zahra (a.s) katika Uislamu.

Programu hiyo ilitumika kama ukumbusho wa umuhimu wake unaoendelea kwa wanawake na wasichana vijana, na nafasi yake kama mfano wa maadili, subira, uchamungu na ujasiri wa kusimamia haki.

Hafla hiyo, iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya watu, ilipambwa na uwepo wa Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nairobi, Dkt. Ali Gholampour, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni Dkt. Mahdi Beyki, Sheikh Ali Mwega, Mchungaji na Msomi wa Chuo Kikuu cha St. Paul, Rev. Wayua, Mtaalamu wa Masuala ya Utawala, Balozi Esther Waringa, pamoja na wasomi na wageni wengine mashuhuri.

Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Iran Nairobi Laadhimisha Maulid ya Sayyidat Fatima Zahra (s.a), Siku ya Mama na Heshima ya Mwanamke +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha