Akisisitiza umuhimu wa kuunganisha maarifa ya Qur'an na matendo ya kijamii, Rais wa Iran amesema: Tatizo kubwa ni pengo kati ya kuijua na kuitekeleza Qur'an. Tunadai kuwa Qur’an inatuonyesha njia ya uongofu na inamfikisha Mwanadamu katika kilele cha juu zaidi, lakini ikiwa kivitendo hakuna dalili ya mwongozo huu inayoweza kuonekana katika maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii, basi kwa hakika tunapaswa kuangalia upya tabia zetu.
Sheikh Maulid Hussein Kundya amesisitiza juu ya umuhimu wa kuisoma na kuifahamu Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa".