16 Machi 2025 - 18:08
"Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa"

Sheikh Maulid Hussein Kundya amesisitiza juu ya umuhimu wa kuisoma na kuifahamu Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa".

Kwa mujibu wa ripoti la Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -: Leo hii tarehe 16 Machi, 2025, Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa Jijini Arusha, Tanzania, imezindua Kituo muhimu cha Qur'an Tukufu katika maeneo ya Ngarinaro.

Sheikh Maulid Hussein Kundya, Mkuu wa Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa, amesisitiza juu ya umuhimu wa kuzisoma na kuzifahamu Aya za Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli Tukufu ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa". (Suratul-Israa: Aya ya 9).

"Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa"

Samahat Sheikh Maulid Hussein Kundya, akizindua Kituo hiki, ameashiria juu ya malengo ya uzinduzi wa Kituo hiki cha Qur'an, nayo ni kama ifuatavyo:

1) Kuunda muktadha unaofaa na jukwaa la kukuza utamaduni wa Qur'an na ukuzaji na upanuzi wa vituo vinavyohusiana na hilo.

2) Kuboresha kiwango cha kiasi na ubora wa uwezo wa kusoma na kuelewa Qur'an Tukufu, na kufaidika iwezekanavyo na Kitabu hiki Kitukufu kinachomjenga Mwanadamu.

3) Kurutubisha (au kufaidika na) muda wa mapumziko wa Wanafunzi kupitia kuisoma na kuifahamu Qur'an.

4) Kuunda mazingira yanayofaa ya kuendesha mafundisho ya Sayansi za Qur'an na Harakati za Qur'an katika utaratibu uliopangwa vizuri, hasa kwa Wanafunzi waliochaguliwa (kujikita zaidi katika masomo ya Qur'an) na ambao wanapenda Sayansi ya Qur'an.

5) Kujenga mazingira ya kufaa ili kuvutia ushiriki zaidi wa matabaka mbalimbali ya watu (katika kujifunza Sayansi za Qur'an / Ulumil Qur'an).

"Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa"

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha