Uzinduzi
-
Sharīatmadār katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili”:
Sayyid Isa Tabatabaei alipuliza roho ya mapambano ndani ya mwili wa jamii ya Kishia / Maadamu kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuwa hai
Balozi wa zamani wa kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: “Ikiwa Imam Musa Sadr alikuwa mwanzilishi wa taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepuliza roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia na kuifanya roho hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wao. Kutokana na jitihada zake, ndipo mapambano ya kisasa ya Lebanon yalipozaliwa - mapambano ambayo baadaye yalifikia kilele chake katika kuunga mkono dhana na malengo ya Palestina.”
-
Iran Yazindua Makombora Mapya Yenye Uwezo wa Kuongozwa Angani
Wataalamu wa kijeshi wanaona kuwa teknolojia ya kuongozwa kwa Makombora yakiwa angani inafanya makombora hayo kuwa na faida kubwa kutokana na uwezo wake wa kurekebisha au kubadilisha mwelekeo kwa wakati halisi na Sahihi, jambo linaloongeza usahihi na kupunguza uwezekano wa kuruka hadi mbali bila kufikia shabaha yake.
-
Jenerali Shakarchi: Uzalishaji wa Makombora ya Iran Hautasimama Kamwe / Uzoefu wa Libya Umeonyesha Kuondoa Silaha Kunaleta Uharibifu Tu
Shakarchi aliongeza: Adui walidhani kuwa kuendelea kwa vita zaidi ya wiki moja kutasababisha uchovu na kuchoshwa kwa watu, lakini ushiriki mkubwa wa umma na msaada usiokatizwa kwa Mapinduzi na mfumo viligonga mipango yao yote na mfululizo wa kushindwa kwao ukaendelea.
-
Uzinduzi wa Kituo cha Qur'an - Arusha, Tanzania:
"Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa"
Sheikh Maulid Hussein Kundya amesisitiza juu ya umuhimu wa kuisoma na kuifahamu Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa".