Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Quran na Hadithi - Zanzibar, limefanyika kwa mafanikio makubwa chini ya uongozi na usimamizi wa Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa, Tanzania - Dr. Ali Taqavi. Wanafunzi wa Jamiatul-Mustafa - Tanzania na vyuo vingine wameshiriki katika Mashindano haya ya Hifdhi ya Quran Tukufu na Hadithi. Hii ni katika kuhuisha utajo wa Qur'an Tukufu, na Harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Qur'an Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja wa Tablighi, kwa kujituma kwa kila jambo ili kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Qur'an na Ahlulbayt (a.) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.
Katika Mashindano haya ya Qur'an Tukufu, Wanafunzi wanashinda katika kuhifadhi Qur'an Tukufu kaanzia Juzuu 3, 5, 7, ... mpaka Juzuu 30. Na washindi katika kila kipengele wanajipatia zawadi nono zenye lengo adhimu la kuzidi kuwahamasisha na kuwashajiisha wazidi kuiweka Qur'an Tukufu katika vifua vyao, na katika Maisha yao ya kila siku, na wahakikishe kuwa wanaishi daima kwa mujibu wa muongozo wa Qur'an Tukufu, kwa hakika Qur'an ni uhai wa nyonyo.
Your Comment