Tamasha hili la Mashindano ya Qur'an Tukufu, ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu, na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Qur'an Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Usimamizi na Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu Amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi na khidma kwa Qur'an Tukufu, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.