Mwenyezi Mungu
-
Hujjat-ul-Islam Aali: Msaada kwa wengine unarudishwa (unafidiwa) mara nyingi zaidi na Mwenyezi Mungu
Mwalimu wa chuo kikuu na shule ya kidini alieleza kuwa kusaidia na kutatua matatizo ya wengine ni chanzo cha kupata malipo mengi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alisisitiza kwamba sehemu ya kila mtu katika neema ya Mwenyezi Mungu inategemea uwezo wake wa kupokea, na ili kufaidika zaidi, ni lazima kuongeza uwezo huu.
-
Hadithi ya Shetani na Mwanadamu:
"Siri ya Muda wa Shetani Kuishi: Kwa Nini Mwenyezi Mungu Alimpa Shetani Muda Mrefu wa Kuishi?
Tangu wakati huo ambapo Shetani aliasi na kukataa kumsujudia Adam (a.s), mzozo wa kihistoria kati yake na Mwanadamu ulianza; mzozo ambao unaendelea hadi leo hii. Lakini swali muhimu ni hili: Kwa nini Mwenyezi Mungu alimpa adui huyu katili (Shetani) muda mrefu wa kuendelea kuishi na kujaribu na kuwapoteza watoto wa Adam (Wanadamu)?!. Nakuletea Hadithi nzuri na yenye mazingitio ndani yake kuhusu Shetani na Mwanadamu, na utaijua sababu na siri ya Ruhusa ya Mwenyezi Mungu kwa Shetani ili aendelee kuishi kwa muda mrefu.
-
Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Qur'an na Hadithi - Zanzibar, Tanzania limefanyika kwa mafanikio makubwa
Tamasha hili la Mashindano ya Qur'an Tukufu, ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu, na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Qur'an Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Usimamizi na Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu Amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi na khidma kwa Qur'an Tukufu, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.
-
Umuhimu wa Hijab kwa Mwanamke: Ni kwa nini Hijab ni Wajibu kwa Mwanamke wa Kiislamu?
Katika zama hizi, Hijabu imelinganishwa na kutoendelea kwa jamii na inafikiriwa kuwa ni ishara ya kifungo cha wanawake. Wahubiri wengi wanafikiria kuwa ni bora kutolizungumzia jambo hili katika majlisi zao. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Inapotokea Bid’ah na Mwanachuoni asikiseme kile akijuacho (dhidi ya Bid’ah hiyo), basi (Mwanachuoni huyo) hulaaniwa na Mwenyezi Mungu, Malaika na Wanadamu.”
-
Kuchapishwa kwa kitabu cha kwanza kuhusu Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah kwa ajili ya Watoto
Kitabu cha kwanza cha Watoto na Vijana kuhusu Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kilichoitwa "Baba Hadi" kilichoandikwa na: Elaheh Akherati, kimechapishwa na sasa kinapatikana kwa wale wanaotaka.
-
Ni kwa namna ipi Sala hukataza maovu?
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema ndani ya Qur'an Tukufu anasema: (اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ). "Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda".
-
Umuhimu wa Qur'an Tukufu katika Maisha yetu kama Wanadamu
Kila Aya katika Aya za Qur’an ni chimbuko la mwangaza, muongozo na rahma, kwa hiyo mwenye kutaka mafanikio ya milele na kuokoka katika dunia yake, basi ni juu yake kushikamana na kitabu cha Mwenyeezi Mungu (s.w) usiku na mchana na kuzifanya Aya za Qur’an Tukufu kuwa mfano katika kumbukumbu zake na kituo cha fikra zake ili awe katika mwangaza wa Mwenyeezi Mungu (s.w).
-
Ujumbe wa Ayatollah Ramezani wa rambirambi kwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Ukaribu wa Madhehebu za Kiislamu
Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) ametoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Baba yake Hojat al-Islam Wal-Muslimin, Dakta Hamid Shahriari.
-
Ufafanuzi wa Dua ya kabla ya Alfajiri 3 | Maimamu (a.s) ni "Neno Kamili" la Mwenyezi Mungu
Dua ya kabla ya alfajiri ikiwa kama dua maarufu zaidi ya kabla ya asubuhi kuingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imepokelewa kutoka kwa Imam Baqir (AS). Uhusiano kati ya dhana ya juu ya Dua hii na nafasi ya Uimamu ni moja ya mada muhimu katika maelezo ya Dua hii.
-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dokta Abubakar Zuber Ali Mbwana:
"Maendeleo sio ugomvi, bali ni kufanya mambo yanayoonekana na yanayompendeza Mwenyezi Mungu"
Msikiti ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ni Kituo cha kiroho, kijamii na kiutamaduni, na vile vile ni nyumba makhsusi kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali ndani yake.