Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- miongoni mwa dua za mvua zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu watoharifu (a.s), Sala na Dua ya Imam Reza (a.s) kutokana na sababu za kisiasa, kiitikadi na kihistoria, ina upekee wa aina yake.
Miongoni mwa vyanzo vya riwaya, dua mbili zimenukuliwa kutoka kwa Imam Reza (a.s) ambazo zote zimekuja katika kitabu Sahifa Jamia Radhawiyya kilichoandikwa na Ayatollah Sayyid Muhammad Baqir Muhaqqiq Abtahi.
Dua ya pili katika matini hii ina ufanano mkubwa na dua za mvua zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu watoharifu (a.s), ambapo miongoni mwa sifa zake ni kuainisha sifa za “mvua inayotakiwa”. Sifa mojawapo ya mvua hii, kama ilivyoelezwa katika dua mbalimbali kwa lafudhi zinazofanana, ni mvua ambayo:
«تُحْیی بِهِ الْعِبادَ وَالْبِلادَ»
Mvua ambayo kwa kupitia hiyo, waja wa Mwenyezi Mungu na ardhi hufufuliwa.
Ni wazi kuwa kinachokusudiwa kufufuliwa kwa watu ni kufufuka kwa itikadi zao, na kuhifadhi uhai wa kiroho ndani yao.
Ama dua ya pili iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Reza (a.s) ambayo imetajwa katika Bihar al-Anwar Juzuu ya 49 ukurasa wa 180, na katika Uyūn Akhbār al-Ridhā Juzuu ya 2 ukurasa wa 172, ndiyo hii:
«اَللّهُمَّ یا رَبِّ اَنْتَ عَظَّمْتَ حَقَّنا اَهْلَ الْبَیْتِ، فَتَوَسَّلُوا بِنا کَما اَمَرْتَ، وَاَمَّلُوا فَضْلَکَ وَرَحْمَتَکَ، وَتَوَقَّعُوا اِحْسانَکَ وَنِعْمَتَکَ، فَاسْقِهِمْ سَقْیا نافِعا عامّا غَیْرَ رائِثٍ وَلا ضائِرٍ، وَلْیَکُنْ اِبْتِداءُ مَطَرِهِمْ بَعْدَ انْصِرافِهِمْ مِنْ مَشْهَدِهِمْ هذا اِلی مَنازِلِهِمْ وَمَقارِّهِمْ»
Ee Mwenyezi Mungu, Ee Mola! Wewe umeutukuza haki yetu sisi Ahlul-Bayt; hivyo watu wametutawassali sisi kama ulivyoamrisha. Wameuamini fadhila yako na rehema zako, na wanasubiri wema wako na neema yako. Basi wanyweshe (mvua) unyweshaji wenye manufaa, wa jumla, usiokuwa na kuchelewa wala madhara. Na mwanzo wa mvua hiyo uwe baada ya wao kuondoka kutoka kwenye eneo hili la mkusanyiko kuelekea katika nyumba zao na makaazi yao.
Miongoni mwa mambo yanayong’ara katika maneno ya dua hii ni kusisitiza tawassul kwa Ahlul-Bayt (a.s), na kubainisha nafasi ya Imam Reza (a.s) kama mmoja wa Ahlul-Bayt (a.s):
«اَللّهُمَّ یا رَبِّ اَنْتَ عَظَّمْتَ حَقَّنا اَهْلَ الْبَیْتِ، فَتَوَسَّلُوا بِنا کَما اَمَرْتَ»
Ee Mwenyezi Mungu, Wewe umetukuza haki yetu sisi Ahlul-Bayt, hivyo watu wametutawassali kama ulivyoamrisha.
Kwa mtazamo wa kihistoria, kauli hii katika zama za utawala wa Bani Abbas — ambao walijinasibisha kuwa ni jamaa wa Mtume (s.a.w.w) na sehemu ya Ahlul-Bayt (a.s) — ilikuwa na malengo maalumu. Hata hivyo, kauli hizi hazibainishi tu ukweli wa kisiasa au historia; bali zinaelezea nafasi ya msingi ya Ahlul-Bayt (a.s) katika mfumo wa uumbaji.
Maneno haya yamenukuliwa pia kutoka kwa baba zake Imam Reza (a.s) mfano Imam Ja’far al-Sadiq (a.s), pamoja na watoto wake kama Imam Hadi (a.s), ndani ya matini mbalimbali za riwaya, yakionyesha sehemu ya nafasi ya Ahlul-Bayt (a.s) katika mfumo wa uumbaji na kushuka kwa mvua.
Kwa mfano, katika Usul al-Kafi, imepokelewa kutoka kwa Imam al-Sadiq (a.s) kwamba:
«بِنَا أَثْمَرَتِ الْأَشْجَارُ وَأَیْنَعَتِ الثِّمَارُ وَجَرَتِ الْأَنْهَارُ وَبِنَا یَنْزِلُ غَیْثُ السَّمَاءِ وَیَنْبُتُ عُشْبُ الْأَرْضِ»
Kwa baraka zetu sisi, miti hutoa matunda, mazao hukomaa, mito hutiririka, mvua hushuka kutoka mbinguni, na mimea huchipuka ardhini.
Aidha, katika ziyara iliyopokelewa kutoka kwa Imam al-Sadiq (a.s) na Sheikh Abbas Qummi akaileta kama Ziyarat Mutlaqa ya Kwanza ya Imam Husayn (a.s) ndani ya Mafatih al-Jinan, imekuja kauli hii:
«بِکُمْ یَکْشِفُ اللهُ الْکَرْبَ وَبِکُمْ یُنَزِّلُ اللهُ الْغَیْثَ»
Mwenyezi Mungu kwa kupitia ninyi (Ahlul-Bayt) huondoa huzuni, na kwa kupitia ninyi mvua hushuka.
Imam Hadi (a.s) naye katika Ziyarat Jami’a Kabira amesisitiza nafasi hiyo adhimu kwa kusema:
«بِکُمْ یُنَزِّلُ الْغَیْثَ»
Mwenyezi Mungu kwa kupitia ninyi hushusha mvua.
@Sayyid Ali-Asghar Hosseini / ABNA
Your Comment