Waziri Mkuu ametoa mfano wa maeneo yanayohusiana na rushwa ikiwa ni michakato ya manunuzi, utiaji saini wa mikataba na makusanyo. Aidha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesisitiza kuwa Sekretarieti ya Maadili ina jukumu kubwa la kuhakikisha nchi inaendeshwa kimaadili.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza umuhimu wa kufanya mapitio ya haraka ya tamko la mali na madeni ya viongozi wa umma na kuunda madaraja ya kipaumbele kwa maeneo yanayokithiriwa na rushwa. Amesema baadhi ya watumishi bado hawajajumuishwa katika mfumo wa uwajibikaji licha ya rushwa kuenea katika baadhi ya sekta.

Dkt. Mwigulu alitoa kauli hiyo alipotembelea Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jijini Dodoma, na kuagiza taasisi hiyo kushirikiana na TAKUKURU ili kuziba mianya yote ya rushwa kupitia ukaguzi wa tamko la mali na madeni. Amesema ni lazima maeneo yenye rekodi za rushwa yapewe kipaumbele, na kwamba fomu za tamko ziwe za ukweli na za kuendana na hali halisi ya kila kiongozi.

Your Comment