Sala ya kuomba mvua ya Imam Reza (a.s) ni miongoni mwa matukio maarufu ya kihistoria ambayo ndani yake, mbali na kusisitiza juu ya kuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu, pia imebainishwa nafasi maalumu ya Uimamu na Ahlul-Bayt (a.s) katika kushuka kwa mvua ya rehema ya Mwenyezi Mungu.
Katika maelezo yaliyojaa mazingatio, khatibu alibainisha kuwa Moto wa Jahannamu una mawe yanayochoma hadi kufikia ubongo wa waliomo ndani yake, na kwamba kila aina ya moto ni adhabu maalumu kwa aina fulani ya dhambi, kama zilivyobainishwa katika Hadithi za Mtume.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Qaraati, akionyesha umuhimu wa malezi ya kidini katika familia na shule, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia jukumu la Chuo cha Walimu, walimu na wazazi katika kuimarisha utamaduni wa sala miongoni mwa kizazi kipya.