Baraka za Mtoto Tumboni na Kuzaliwa: Fatuma Zahra alitambulika kwa baraka za kipekee akiwa tumboni, akimlinda mama yake kutokana na uchovu na wasiwasi. Mara tu alipozaliwa, mtoto aliongea mara moja na kutangaza: "Shahidi nina shahada kwamba hakuna aliye stahiki kuabudiwa isipokuwa Allah na Baba yangu ni Mtume wa Allah." Tarehe ya kuzaliwa kwake ilijaa mwanga wa kiroho na nuru ya ulimwengu mzima, ikionyesha umuhimu wake wa kipekee katika historia ya Uislamu.

11 Desemba 2025 - 17:37

Sherehe ya Kuzaliwa kwa Bibi Fatuma Zahra (A.S) Yafanyika Nchini Malawi kwa Mwanga, Baraka na Mafundisho ya Kiimani

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, Tarehe 11 Disemba, 2025, Hafla ya Kuzaliwa kwa Sayyidat Fatima Zahra (sa) katika shule (Hawzat) ya Al-Hadi, Nchini Malawi, Chini ya Harakati za Kitamaduni za Jamiatul - Mustafa (s), ikiongozwa na Rais wake Dkt. Ali Taqavi. Wanafunzi na walimu walikusanyika katika Hafla hiyo ili kusherehekea kuzaliwa kwa Bibi huyu Mtukufu, Kipenzi cha Mtume wetu Muhammad (saww), Hazrat Fatuma Zahra (A.S),  na ambaye pia ni mke wa Imam Ali (a.s) na mama wa Maimamu Wawili Watukufu Imam Hassan na Imam Hussein (Amani iwe juu yao). Khutba ya Mnasaba huu ilitolewa na Sheikh Abdulrashid Shaib ambapo alisitiza nafasi ya kiroho na kifamilia ya Sayyidat Fatima Zahra,(sa) na kutoa mwangaza juu ya maadili, utii wa dini na kuwa kwake mfano hao wa kielelezo kwa Waislamu na Waumini wa kila wakati na kila Zama.

Khutba hiyo ilijikita katika vipengele vifuatavyo:

  1. Ujauzito wa Bibi Khadija (A.S): Sheikh Shaib alielezea hali ya ujauzito wa Bibi Khadija wakati alipokuwa akijifungua Fatuma Zahra, na jinsi mtoto alivyoleta amani kwa mama yake katika kipindi chote cha ujauzito.

  2. Baraka za Mtoto Tumboni na Kuzaliwa: Fatuma Zahra alitambulika kwa baraka za kipekee akiwa tumboni, akimlinda mama yake kutokana na uchovu na wasiwasi. Mara tu alipozaliwa, mtoto aliongea mara moja na kutangaza:
    "Shahidi nina shahada kwamba hakuna aliye stahiki kuabudiwa isipokuwa Allah na Baba yangu ni Mtume wa Allah."
    Tarehe ya kuzaliwa kwake ilijaa mwanga wa kiroho na nuru ya ulimwengu mzima, ikionyesha umuhimu wake wa kipekee katika historia ya Uislamu.

  3. Baraka za Kipekee: Sheikh Shaib aliongeza kuwa Fatuma Zahra alizaliwa kutoka tone la maji ya tufaa ya Peponi, ikionyesha asili yake ya kipekee na utelezi wa baraka.

  4. Kielekezi cha Kiimani: Fatuma Zahra ni mfano wa kiimani na kimaadili. Sheikh Shaib alisisitiza kuwa heshima yake si kwa sababu ya kuwa binti ya Mtume wa Allah pekee, bali kwa utii wake wa dini, adabu, na ibada zake za kiroho.

  5. Upendo na Baraka: Kupendwa na kuiga Fatuma Zahra kunaleta thawabu na baraka za kiroho kwa wapendwa wake, na kuonyesha jinsi utii na mapenzi kwa wafuasi wa njia yake unavyoongeza thawabu katika maisha ya kiroho.

  6. Majina na Vyeo Vyake: Sheikh Shaib alitaja majina na vyeo vya Fatuma Zahra, akiwemo “Sayyidat Nisa al-Alamin” – Mhebu wa Wanawake wa Dunia. Aidha, alibainisha nafasi yake ya kipekee kama mama wa wa-Imamu, mke wa Imam Ali (A.S), na binti wa Mtume Muhammad (S.A.W.W).

    Sherehe ya Kuzaliwa kwa Bibi Fatuma Zahra (A.S) Yafanyika Nchini Malawi kwa Mwanga, Baraka na Mafundisho ya Kiimani

Hafla hii ilisisitiza ukubwa wa nafasi ya Bibi Fatuma Zahra (A.S) katika maisha ya kiroho na kifamilia, na kuhimiza waumini kuiga mfano wake wa utii wa dini, ibada, haki, na adabu. Sheikh Shaib alisisitiza kuwa kutambua na kuiga baraka na maisha ya Fatuma Zahra ni njia ya kupata mwanga na mafanikio ya kiroho kwa vizazi vyote.

Sherehe ya Kuzaliwa kwa Bibi Fatuma Zahra (A.S) Yafanyika Nchini Malawi kwa Mwanga, Baraka na Mafundisho ya Kiimani

Your Comment

You are replying to: .
captcha