Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran, Dkt. Mehdi Beigi, leo amefanya kikao cha ufuatiliaji na viongozi wa APBET SAK kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya ajenda ya mambo manne yaliyokubaliwa awali kati ya viongozi wa APBET SAK–Kanda ya Nairobi na Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Iran. Kikao hicho pia kimejadili fursa zaidi za ushirikiano, ikiwemo kubadilishana walimu na kujenga uwezo katika maeneo mbalimbali ya elimu.

APBET (Alternative Provision of Basic Education and Training) ni shule za gharama nafuu nchini Kenya zinazolenga watoto wanaoishi katika maeneo yaliyotengwa kama vile mitaa ya mabanda, makazi duni, na maeneo kame au yenye ukame (ASALs). Shule hizi zimeanzishwa ili kuwafikia watoto wanaokosa nafasi katika mfumo rasmi wa elimu, kwa kuwapatia elimu ya msingi na mafunzo muhimu. APBET pia hutetea kutambuliwa na kuungwa mkono na Serikali kwa ajili ya uandikishaji, uboreshaji wa kiwango cha elimu, na kuhakikisha watoto wote wanapata fursa sawa za elimu bora bila ubaguzi.

Your Comment