utekelezaji
-
Iran: Kuieleza UN kama chombo cha kuzuia vita kati ya mataifa yenye nguvu ni tafsiri potofu na hatari
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amesema kuwa kuifanya falsafa ya kuwepo kwa Umoja wa Mataifa (UN) ionekane kuwa ni kuzuia tu kuzuka kwa vita kati ya mataifa yenye nguvu ni tafsiri potofu na hatari.
-
Robert Kagan: Mataifa ya Ghuba Hayana Ari Tena ya Kukaribisha Kambi za Kijeshi za Marekani
Mchambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa Robert Kagan amesema serikali za nchi za Ghuba ya Uajemi hazina utayari kama zamani wa kuwa wenyeji wa kambi za kijeshi za Marekani, zikieleza kutoridhishwa na kiwango cha ulinzi wa kiusalama kinachotolewa na Washington.
-
Iran: Mazungumzo na Oman ni ya Pande Mbili, Hayawahusu Wadau Wengine
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa mazungumzo kati ya Iran na Oman ni ya pande mbili na hayahusiani na upande mwingine wowote, akisisitiza kuwa msimamo wa Iran kuhusu Mlango wa Hormuz na maslahi yake ya kitaifa hautabadilishwa na vitisho au shinikizo.
-
Iran: Utekelezaji wa Makubaliano na Marekani Unategemea Kutekelezwa kwa Ahadi za Washington | Makubaliano hayo Yamekwisha baina ya Iran na Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuwa utekelezaji wa makubaliano yoyote na Marekani unategemea Washington kutekeleza kikamilifu ahadi zake, huku ikisisitiza kuwa hakuna shaka kuwa makubaliano ya awali ya hati ya maelewano (Memorandum of Understanding) yamefikia mwisho.
-
Kwa Mujibu wa ABNA: Ujumbe wa Iran na Makamu wa Rais wa Marekani Wawasili Uswisi kwa Mazungumzo Muhimu
Ujumbe wa Iran umefika Uswisi kwa mazungumzo kuhusu Makubaliano ya Islamabad, huku Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, naye akiwasili kushiriki katika duru hiyo ya mazungumzo.
-
Gharib Abadi: Nguvu za Kijeshi za Iran Zililazimisha Adui Kuketi Mezani; Hati ya Mwisho ya Makubaliano Yakamilika
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Gharib Abadi, amesema nguvu za kijeshi za Iran ndizo zilizomlazimisha adui kurejea kwenye mazungumzo, akisisitiza kuwa maandishi ya mwisho ya hati ya maelewano yamekamilika na kutiwa saini rasmi kutafanyika Ijumaa nchini Uswisi, huku Iran ikiahidi kujibu hatua yoyote ya kutotekelezwa kwa ahadi za upande wa pili.
-
Mbunge wa Hizbullah: Israel Itaondoka Kusini mwa Lebanon kwa Mujibu wa Makubaliano kati ya Marekani na Iran
Mbunge wa Hizbullah amesema Lebanon itakuwa sehemu ya makubaliano yoyote ya usitishaji vita, akisisitiza kuwa kuondoka kwa majeshi ya Israel kusini mwa Lebanon na dhamana za Marekani ni masharti muhimu ya utekelezaji wake.
-
Kenya - Nairobi | Mazungumzo ya Kiutamaduni: Ubalozi wa Iran na APBET SAK Waimarisha Mafungamano ya Kielimu
APBET (Alternative Provision of Basic Education and Training) ni shule za gharama nafuu nchini Kenya zinazolenga watoto wanaoishi katika maeneo yaliyotengwa kama vile mitaa ya mabanda, makazi duni, na maeneo kame au yenye ukame (ASALs).
-
Barua ya Iran, Urusi na China kwa Grossi: Wajibu wa Kuripoti wa IAEA Umefikia Mwisho
Wawakilishi wa kudumu wa Iran, Urusi na China katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) wamemwandikia barua rasmi Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo, wakisisitiza kuwa kwa kumalizika kwa muda wa utekelezaji wa Azimio la 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jukumu la IAEA la kuwasilisha ripoti chini ya azimio hilo limefikia mwisho, na kwamba hatua yoyote mpya katika mwelekeo huo haina uhalali wa kisheria.