Maeneo
-
Utafiti unaonyesha kuwa maeneo ya nyuklia ya Iran yaliyoshambuliwa na Marekani bado yanafanya kazi kama kawaida - Iran iliwahadaa na kutoa kila kitu
"centrifuges" (au kwa kiswahili: Visukuma ambavyo hutumika katika teknolojia ya nyuklia) zote ziko salama, na ambazo hutumiwa kimsingi kwa urutubishaji wa uranium, mchakato ambao hutenganisha isotopu za uranium ili kuongeza mkusanyiko wa U-235, ambayo huhitajika kwa vinu vya nyuklia.
-
Baqaei: Kushambulia hospitali ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhalifu wa kivita
Akilaani shambulio la kombora la utawala haramu wa Kizayuni katika Hospitali na Kituo cha Tiba cha Farabi huko Kermanshah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ameandika: "Mashambulizi dhidi ya hospitali pamoja na mashambulizi katika maeneo ya makazi ya watu ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na jinai ya kivita."
-
Mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika baadhi ya Makazi ya raia Jijini Tehran
Katika siku ya tatu ya uvamizi wake dhidi ya nchi yetu, utawala haramu wa Kizayuni ulilenga baadhi ya maeneo ya Tehran katika mfululizo wa mashambulizi makali.
-
Wimbi kali la Mashambulizi ya Makombora ya Iran linaendelea katika awamu ya 3 ya Ahadi ya Kweli 3 /Makazi ya Netanyahu na maeneo kadhaa ya kistratijia
Ikinukuu vyanzo vyake vya kijeshi, Redio ya Jeshi la Israel ilithibitisha kurushwa zaidi ya Makombora 50 ya Balistiki kutoka ardhi ya Iran, na ving'ora vya kengele ya hali ya hatari vilisikika katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.
-
Chaguzi za Lebanon chini ya kivuli cha uvamizi wa Israel: Kura kwa chaguo la upinzani (Muqawamah) ndio jambo la msingi na lililopewa kipaumbele
Ingawa jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi makali kusini mwa Lebanon, watu wa eneo hilo walihudhuria uchaguzi wa maeneo kwa wingi, wakithibitisha tena msaada wao kwa harakati za upinzani.
-
Mamlaka za Israeli zimethibitisha kukamatwa kwa raia wawili wa Israeli kwa tuhuma za kufanya ujasusi kwa niaba ya Iran
Watu wawili waishio katika mji wa Haifa wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi kwa niaba ya Iran.