15 Juni 2025 - 18:22
Wimbi kali la Mashambulizi ya Makombora ya Iran linaendelea katika awamu ya 3 ya Ahadi ya Kweli 3 /Makazi ya Netanyahu na maeneo kadhaa ya kistratijia

Ikinukuu vyanzo vyake vya kijeshi, Redio ya Jeshi la Israel ilithibitisha kurushwa zaidi ya Makombora 50 ya Balistiki kutoka ardhi ya Iran, na ving'ora vya kengele ya hali ya hatari vilisikika katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, katika muendelezo wa jibu madhubuti la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hujuma za kuendelea za utawala wa Kizayuni, wimbi jipya la mashambulizi ya makombora ya Iran katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu limeanza saa chache zilizopita. Makombora ya hali ya juu yamerushwa kutoka sehemu tofauti za ardhi ya Iran kuelekea shabaha za kimkakati katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na milipuko mikubwa imeripotiwa katika miji ya Jerusalem, Tel Aviv na Haifa.

Vyanzo vya habari vilitangaza kwamba miji ya Ashkelon, Tel Aviv, na Haifa ilikuwa katikati ya mashambulizi haya. Idhaa ya 12 ya Israel, ikikiri kukithiri kwa mashambulizi hayo, iliripoti milipuko iliyofuatana katika Jerusalem (QUDS) inayokaliwa kwa mabavu na kuelezea anga katika mji huo kuwa katika hali mbaya.

Ikinukuu vyanzo vya kijeshi, Redio ya Jeshi la Israel ilithibitisha kurusha zaidi ya makombora 50 ya balistiki kutoka ardhi ya Iran, na ving'ora vilisikika katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu. Mashambulizi hayo yamepiga mifumo ya ulinzi ya Israeli, ambayo kwa miaka mingi ilijionyesha kuwa haiwezi kupenyeka.

Duru za habari za lugha ya Kiebrania zimeripoti kuwa operesheni hiyo ililenga Makazi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa jinai wa utawala wa Kizayuni na kituo cha kuzalisha umeme cha Al-Khudeira. Hatua hii ni ujumbe wa wazi kwa viongozi wa utawala huo ghasibu kwamba hakuna sehemu yoyote ya ardhi inayokaliwa kwa mabavu iliyo salama kuweza kukwepa uwezo wa makombora wa Iran na muhimili wa Muqawamah.

Operesheni hiyo yenye nguvu inatekelezwa katika hali ambayo utawala haramu wa Kizayuni umekuwa ukihatarisha uthabiti wa eneo hili la kikanda kwa miaka mingi kwa vitendo vyake vya kivamizi vikiwemo mashambulizi dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na ukiukaji wa kujitawala wa nchi za eneo la kikanda. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba uchokozi wowote wa utawala wa Kizayuni utakabiliwa na jibu kali na la uhakika.

Kwa kuanza duru hii ya mashambulizi, vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa Iran kufanya mashambulizi mchana kweupe, na hayo ni maendeleo makubwa na ya hatari.

Kulingana na ripoti ya mwandishi wa Al-Hadath kutoka kwa habari ya kwanza juu ya majeruhi wa shambulizi la makombora la Iran, kulingana na huduma za dharura za Israeli, Waisraeli 500 wamejeruhiwa na watu 12 wameuawa hadi sasa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha