Jeshi la Missili la Jeshi la Silaha la Yemen limetekeleza operesheni ya kijeshi ikilenga Kituo cha Anga cha Nevatim katika eneo la Negev, kusini mwa Palestina iliyokaliwa, kwa kutumia kombora la hipersoniki la balistiki.
Kwa kutoa taarifa rasmi, Hezbollah ya Lebanon imekanusha uhusiano wowote na operesheni hiyo ya makombora leo asubuhi (Jumamosi) dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa, madai ya adui yanalenga kutoa visingizio vya kuendelea na uvamizi.