21 Juni 2025 - 14:12
Gazeti la Wall Street Journal: Israel haiwezi kumudu zaidi ya wiki mbili kwenye vita na Iran

Gazeti hili pia limeelezea kwa kina gharama za vita vya Israel, likisema kuwa gharama za kuzuia kila roketi la Iran kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa angani ya Israel zitakuwa kati ya Dola laki saba (700,000) hadi Dola Milioni Nne (4).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gazeti la Marekani la Wall Street Journal limeonyesha kuwa vita vya Israel dhidi ya Iran vinaigharimu angalau dola bilioni 12 kila mwezi, na limetangaza kuwa Tel Aviv haiwezi kumudu vita kwa kubakia vitani na Iran zaidi ya wiki mbili.

Gazeti hili pia limeelezea kwa kina gharama za vita vya Israel, likisema kuwa gharama za kuzuia kila roketi la Iran kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa angani ya Israel zitakuwa kati ya Dola laki saba (700,000) hadi Dola Milioni Nne (4).

Vilevile, Wall Street Journal limezungumzia gharama za mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa makombora kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Operesheni ya "Al_Wa'd Al_Sadiq 3 / Ahadi ya Kweli 3", likisisitiza kuwa Waarabu wa Israeli wanahitaji angalau dola milioni 400 kwa ajili ya kurejesha mfumo wa miundombinu na majengo yaliyoharibiwa kwa Makombora ya Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha