Gazeti hili pia limeelezea kwa kina gharama za vita vya Israel, likisema kuwa gharama za kuzuia kila roketi la Iran kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa angani ya Israel zitakuwa kati ya Dola laki saba (700,000) hadi Dola Milioni Nne (4).
Kwa kutoa taarifa rasmi, Hezbollah ya Lebanon imekanusha uhusiano wowote na operesheni hiyo ya makombora leo asubuhi (Jumamosi) dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa, madai ya adui yanalenga kutoa visingizio vya kuendelea na uvamizi.