gazeti
-
Uchambuzi wa New York Times;
Je, , Beirut inaweza kuipokonya silaha Hezbollah ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025?
Wachambuzi wanaonya kuwa ikiwa Beirut itaharakisha zoezi la kuipokonya silaha bila kupata mafanikio sambamba kutoka kwa Israel - kama vile kusitishwa kwa mashambulizi ya anga- hatua hiyo inaweza kuimarisha nafasi ya kisiasa na kijamii ya Hezbollah. Hii ni kwa sababu Hezbollah si kundi la kijeshi pekee, bali pia ni chama cha kisiasa chenye ushawishi mpana.
-
Baghdad yafuatilia kuongezeka kwa uwepo wa ISIS
Wasiwasi wa kiusalama nchini Iraq kuhusu shughuli za ISIS mpakani na Syria umeongezeka, licha ya hatua kali za kiusalama, huku kukiwa na maonyo ya kiintelijensia na ongezeko la tahadhari.
-
Utawala wa Kizayuni: Hezbollah imerejesha uwezo wake wa kijeshi katika sehemu kubwa ya majimbo ya mapigano (Mapambano)
Maafisa wa Israel wametoa tahadhari kwamba Hezbollah, kwa msaada wa kifedha kutoka Iran, imefanikiwa kurejesha uwezo wake wa kijeshi na sasa inachukuliwa kuwa tishio la kimkakati kwa Tel Aviv.
-
Daesh wabeba jukumu la shambulio dhidi ya doria ya wanamgambo wa Jolani
Daesh wametekeleza tukio la kushambulia doria inayohusiana na idara ya forodha ya Serikali ya Jolani na kuua watu wawili.
-
Kikundi cha “Abu Shabab” Kusini mwa Ukanda wa Gaza kiko katika hali ya kusambaratika
Kikundi cha wanamgambo kinachoitwa “Abu Shabab” kiko karibu kabisa kuvunjika baada ya kupoteza msaada wa anga kutoka kwa Israel na kushambuliwa kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa Harakati ya Hamas.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atazuru Qatar kesho
Gazeti la Washington Post, likinukuu maafisa wawili wa serikali ya eneo hilo, limeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anatarajiwa kufanya ziara nchini Qatar kesho, siku ya Jumanne.
-
Kuzidi kwa mivutano kati ya Tel Aviv na mhimili wa Ikhwan | Tishio la Uturuki la Shambulio la Kijeshi
Gazeti la Haaretz pia limeitaja Uturuki kuwa shabaha inayofuata zaidi ya Israel na limeonya kuhusu athari mbaya zitakazotokana na hilo.
-
Wayemen hawawezi kushindwa
Gazeti la Kizayuni Jerusalem Post, katika ripoti yake, limesisitiza kuwa Taifa la Yemen haliwezi kushindwa na likabainisha wazi kuwa Israel haitaki vita vya moja kwa moja na Yemen.
-
Gazeti la Wall Street Journal: Israel haiwezi kumudu zaidi ya wiki mbili kwenye vita na Iran
Gazeti hili pia limeelezea kwa kina gharama za vita vya Israel, likisema kuwa gharama za kuzuia kila roketi la Iran kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa angani ya Israel zitakuwa kati ya Dola laki saba (700,000) hadi Dola Milioni Nne (4).