28 Agosti 2025 - 22:35
Wayemen hawawezi kushindwa

Gazeti la Kizayuni Jerusalem Post, katika ripoti yake, limesisitiza kuwa Taifa la Yemen haliwezi kushindwa na likabainisha wazi kuwa Israel haitaki vita vya moja kwa moja na Yemen.

Kwa Mujibu wa Habari ya Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, gazeti la Kizayuni Jerusalem Post limeandika katika ripoti yake kuwa: Tangu mwezi Oktoba 2023, (utawala wa) Israel umeshindwa kuzuia mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka kwa Wayemen.

Gazeti hilo limeongeza kuwa: Israel tangu mwanzo haikutaka kuingia vitani moja kwa moja na Yemen, na ilijaribu kuhamishia suala hilo kwa Marekani.

Jerusalem Post, ikinukuu maafisa waandamizi wa utawala wa Kizayuni, linasema: Wayemen ni kati ya wapiganaji wa kichaa zaidi katika eneo hili, na kupambana nao ni jambo baya sana kwa Israel, kwa sababu hawashindiki.

Gazeti hilo limeeleza pia kuwa: Maafisa wa Marekani wameunga mkono madai ya Israel kwamba Wayemen hawawezi kushindwa.

Gazeti linaendelea: Maafisa wa Israel walijisifu kuwa mji mkuu wa Yemen, Sana'a, utabaki bila umeme kwa muda mrefu, lakini Wayemen walifanikiwa kurejesha umeme kwa muda mfupi na hata wakarusha kombora lingine jipya kuelekea Israel.

Aidha, likinukuu vyanzo ndani ya jeshi la Israel, gazeti limeandika: Yemen ni changamoto kubwa, na taasisi za kijasusi za Israel zinafanya jitihada kutafuta suluhisho dhidi ya tishio hilo.

Jerusalem Post pia limeongeza kuwa: Uamuzi wa Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, kusitisha vita dhidi ya Yemen uliiacha Israel peke yake ikikumbana na dhoruba.

Na hatimaye, kwa mujibu wa gazeti hilo: Jeshi la Israel linaamini kuwa lazima waikabili Yemen hatua kwa hatua, lakini kupenya kijasusi ndani ya Yemen ni jambo linalohitaji muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa.

Gazeti linahitimisha kwa kusema: Kusimamishwa kwa vita katika Ukanda wa Gaza kutasababisha kusitishwa kwa mashambulizi ya makombora kutoka Yemen.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha