“Umma wa Malk Khashab,” Mwanahabari wa kike wa Ansarullah, aliandika:
Katika mapambano kati ya wavamizi na Wazayuni dhidi ya Yemen, hesabu zote zimebadilika na mizani imegeuzwa. Kwa hivyo, walianza kulia na kupiga kelele kutokana na wanaume imara wa Yemen na wana-yemen kwa ujumla, na sasa Yemen imekuwa moto wa kuotea mbali na ndoto za kutisha kwao zinazowaamsha mara kwa mara.
Gazeti la Kizayuni Jerusalem Post, katika ripoti yake, limesisitiza kuwa Taifa la Yemen haliwezi kushindwa na likabainisha wazi kuwa Israel haitaki vita vya moja kwa moja na Yemen.