Gazeti la Kizayuni Jerusalem Post, katika ripoti yake, limesisitiza kuwa Taifa la Yemen haliwezi kushindwa na likabainisha wazi kuwa Israel haitaki vita vya moja kwa moja na Yemen.
Amos Malka, aliyewahi kuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi, pia alitoa onyo kuwa:"Tuko karibu na ukingo wa kushindwa. Malengo ya awali ya kijeshi yalitimia muda mrefu uliopita, lakini kwa sababu za kisiasa – si za kijeshi – mapigano yanaendelea, na hali hii inaiathiri vibaya Israel kisiasa na kiusalama."