5 Desemba 2025 - 15:21
Daesh wabeba jukumu la shambulio dhidi ya doria ya wanamgambo wa Jolani

Daesh wametekeleza tukio la kushambulia doria inayohusiana na idara ya forodha ya Serikali ya Jolani na kuua watu wawili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa limechukua jukumu la shambulio lililolenga doria inayohusiana na Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya serikali ya al-Jolani. Shambulio hilo lilifanyika jioni ya Jumatano na wanachama wa kundi hilo, na taarifa hiyo ilitangazwa kupitia akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Al-Araby Al-Jadeed, kwa madai ya kundi hilo, washambuliaji waliweza kuua wanachama wawili wa doria ya serikali ya Jolani karibu na mji wa Al-Zarbah, katika viunga vya mkoa wa Aleppo, kwenye barabara ya Aleppo – Damascus, na watu wengine wawili walijeruhiwa.

Kwa upande mwingine, vyanzo vya eneo hilo vililiambia gazeti la Al-Araby Al-Jadeed kuwa “Issa Raad”, mmoja wa waliouawa katika shambulio hilo, alizikwa mchana wa Alhamisi katika mji wa Al-Qusayr, katika viunga vya mkoa wa Homs.

“Mazen Alloush”, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa Idara ya Mkuu ya Forodha ya serikali ya Jolani, aliandika katika mtandao wa X (zamani Twitter) akieleza kuwa: Shambulio hilo lililenga doria iliyokuwa na jukumu la kusindikiza lori, ambapo doria hiyo ilinasa katika mtego wa silaha katika eneo la Al-Zarbah, kusini mwa viunga vya Aleppo, kupitia gari lililokuwa limebeba watu wenye silaha.

Akaongeza kuwa: Shambulio hilo lilipelekea vifo vya watu wawili wa vikosi vya forodha na wengine wawili kujeruhiwa.

Ikumbukwe kuwa awali pia Daesh ilifanya shambulio kama hilo, ambapo iliwaua watu wawili wa Wizara ya Ulinzi ya serikali ya Jolani katika maeneo ya mji wa Saraqib, katika viunga vya mkoa wa Idlib. Shambulio hilo lilitokea katika wiki ya mwisho ya mwezi Novemba.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha