Tukio
-
Katika mahojiano na ABNA na mwanafalsafa wa Marekani: Kutoka ‘Medina’ hadi New York; Kushindwa kwa Ukuta wa Hofu Dhidi ya Uislamu Marekani
Profesa Charles Taliaferro, profesa mwandamizi wa falsafa katika Chuo cha Saint Olaf, akitaja wimbi la kampeni za propaganda za kupinga Uislamu nchini Marekani, alisema: “Licha ya kuwepo kwa baadhi ya vipengele vya kupinga Uislamu katika jamii ya Marekani, kuna ishara wazi za heshima, utu, na kukubaliana kati ya Waislamu na watu wengine. Ushindi wa Zahran Mamdani katika uchaguzi wa manispaa ya New York ni tukio muhimu katika kuimarisha harakati za kudhoofisha mazungumzo ya hofu dhidi ya Uislamu.”
-
Msimu wa Mizeituni Umekuwa Msimu wa Mauaji katika Ukingo wa Magharibi | Ukandamizaji na mashambulizi ya wakoloni wa Kizayuni yaongezeka kwa ukatili
Msimu wa mavuno ya mizeituni - ishara ya amani na ustawi kwa Wapalestina - umegeuzwa na utawala wa Kizayuni kuwa msimu wa hofu, damu na uharibifu. Ukandamizaji na mashambulizi ya wakoloni wa Kizayuni yaongezeka kwa mpangilio na ukatili mkubwa
-
Spika wa Bunge la Iran: "Iran Haitaikubali Utawala wa Kigeni"
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, ameweka wazi kuwa taifa la Iran halitawahi kukubali kutawaliwa na mataifa ya kigeni na litalinda uhuru wake kwa gharama yoyote.
-
Watu 2 wameuawa katika shambulio la silaha mbele ya sinagogi ya Kiyahudi huko Manchester, Uingereza
Tukio lililotokea sambamba na sherehe ya Yom Kippur mbele ya sinagogi ya Kiyahudi huko Manchester, Uingereza, limesababisha vifo vya watu 2 na kujeruhi wengine 3.
-
Hakim: Kimya mbele ya uvamizi wa Israel hakikubaliki
Sayyid Ammar Hakim amesema kuwa ujasiri wa hali ya juu na dharau ya wazi ya utawala wa Kizayuni katika kuvamia nchi za Kiarabu na Kiislamu, na kutenda jinai za kila siku dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Syria, Lebanon, Yemen, Iran na Qatar ni jambo ambalo kimya dhidi yake hakikubaliki.
-
Watu 55 wauawa katika shambulio la kigaidi kaskazini Mashariki mwa Nigeria
Mmoja wa walionusurika, Malam Bukar, alisema: "Walivamia kijiji wakipiga mayowe na kuanza kuwashambulia watu kiholela. Tuliporudi asubuhi, miili ya watu ilikuwa imetapakaa kila mahali."
-
Ilibainishwa katika mkutano na waandishi wa habari:
Maonesho ya Picha 'Siku 12 za Iran' Tukio Kubwa la Simulizi ya Vita, Yataoneshwa Nchini 40
Maonyesho ya Picha ya Kimataifa “Siku 12 za Iran” yenye mada ya Simulizi Halisi ya Vita vya Kulazimishwa vya Siku 12, yanayoratibiwa na Jumuiya ya Amani ya Kiislamu Duniani na Taasisi ya Utamaduni, Sanaa na Utafiti ya Saba, kwa ushirikiano wa Taasisi 21 za ndani na kimataifa, yatafanyika kuanzia tarehe 14 Septemba katika Taasisi ya Sanaa na sambamba na nchi 40 duniani.
-
Arubaini ya Imam Hussein (a.s):
Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu
Tukio hili limeonesha mshikamano wa kijamii na mshikikano wa kiimani kwa kuenzi mfano wa kujitolea na ubinadamu wa Imam Hussein (a.s), na limekuwa ni ishara muhimu ya mshikamano wa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla katika kusaidia wenzao wenye uhitaji wa Damu Mahospitalini.
-
Sheikh Dr. Alhad Musa Salum Akabidhiwa Tuzo ya Uongozi wa Mfano na JMAT Mkoa wa Dar -es- Salaam
Tukio hilo lilifanyika katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa JMAT kwa Muhula wa Kwanza wa Mwaka 2025, ambapo viongozi mbalimbali wa kidini na kijamii walihudhuria.