17 Agosti 2025 - 16:50
Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Tukio hili limeonesha mshikamano wa kijamii na mshikikano wa kiimani kwa kuenzi mfano wa kujitolea na ubinadamu wa Imam Hussein (a.s), na limekuwa ni ishara muhimu ya mshikamano wa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla katika kusaidia wenzao wenye uhitaji wa Damu Mahospitalini.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Dar -es- Salaam - Tanzania, Leo hii, Tarehe 17-08-2025 - Katika Muktadha wa kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliyeuawa Kishahidi katika ardhi ya Karbala akitetea Haki, Uadilifu, Utu na Heshima ya Ubinadamu, Taasisi za Kijamii zimeandaa tukio muhimu la kijamii na kibinadamu la uchangiaji damu.

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Taasisi hizo za Kijamii zilizoratibu na kuandaa tukio hili ni: (BEF) Beyond Ethnicity Foundation (Taasisi ya Kupita Mipaka ya Ukabila) kwa kushirikiana na (NF) Nyota Foundation, chini ya udhamini wa Care Aid Africa Foundation, na limefanyika katika maeneo ya Chekechea, Mikwambe, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam - Tanzania.

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Washiriki na Ushiriki wa Jamii

Wananchi wengi walijitokeza kwa moyo wa upendo na huruma, wakichangia damu kwa ajili ya Watanzania wenzao wenye uhitaji mkubwa wa damu Hospitalini.

Wataalamu wa Afya Walioshiriki

Zoezi la ukusanyaji damu lilitekelezwa na wataalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Vijibweni, Manispaa ya Kigamboni, kwa kushirikiana na Kitengo cha Damu Salama.

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Bw. Xavery Kapinga, Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Vijibweni, Halmashauri ya Kigamboni, alieleza sifa muhimu za mchangiaji damu, ambapo amezitaja sifa hizo kama ifuatavyo:

1. Awe na Umri kati ya miaka 18–68.

2. Awe na Afya njema na uzito usiopungua kilo 50.

3. Asiwe ni mwenye Kuathirika na magonjwa ya kudumu (kama kisukari, shinikizo la damu) au ya kuambukiza (kama vile UKIMWI) n.k.

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Umuhimu wa Uchangiaji Damu

Akibainisha umuhimu wa uchangiaji damu, Bw. Kapinga alisema:

"Mama wajawazito hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua, hivyo huhitaji msaada wa damu kwa uharaka. Waathirika wa ajali mara nyingi hupoteza damu nyingi na kuhitaji msaada wa haraka wa Damu. Wagonjwa wa selimundu (sickle cell) wanahitaji msaada wa damu mara kwa mara kutokana na changamoto ya muda mrefu kwenye seli nyekundu za damu".

Kwa ujumla, tukio hili limeonesha mshikamano wa kijamii na mshikikano wa kiimani kwa kuenzi mfano wa kujitolea na ubinadamu wa Imam Hussein (a.s), na limekuwa ni ishara muhimu ya mshikamano wa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla katika kusaidia wenzao wenye uhitaji wa Damu Mahospitalini.

Taasisi za Kijamii Nchini Tanzania: BEF na Nyota Foundation Zandaa Tukio la Uchangiaji Damu kwa Upendo na Huruma ya Kibinadamu

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha