Makumi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina wameuawa na kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuwafyatulia risasi wakiwa kwenye Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika Mji Mkuu wa Nigeria.
Imam Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikutana na maelfu ya Wanafunzi wa vyuo vikuu, wawakilishi kutoka Jumuiya za Wanafunzi wa Kisiasa, Kijamii na Kiutamaduni na makundi mbalimbali ya Jihadi. Mkutano huo ulifanyika katika Husseiniyyah ya Imamu Khomeini (MA), mnamo Machi 12, 2025.