22 Oktoba 2025 - 09:46
Gari yagongana na Kizuizi cha Usalama Mbele ya Ikulu ya White House + Picha

Maafisa wa Marekani wametangaza kuwa jioni ya Jumanne wamemkamata mwanaume mmoja baada ya gari lake kugongana na kizuizi cha usalama kilichoko mbele ya lango la kuingilia Ikulu ya White House.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as)-ABNA- Maafisa wa Marekani wametangaza kuwa jioni ya Jumanne wamemkamata mwanaume mmoja baada ya gari lake kugongana na kizuizi cha usalama kilichoko mbele ya lango la kuingilia Ikulu ya White House.

Kulingana na taarifa ya Huduma ya Siri ya Marekani, tukio hilo lilitokea saa 4:37 usiku kwa saa za eneo, na mtu huyo alikamatwa mara moja baada ya kugongana na lango la usalama lililoko kwenye mlango wa kuingilia Ikulu ya White House.

Baada ya kukamatwa, maafisa wa usalama walilikagua gari hilo na kuthibitisha kuwa halikuwa na tishio lolote la kiusalama na lilikuwa salama kabisa.

Gari yagongana na Kizuizi cha Usalama Mbele ya Ikulu ya White House + Picha

Hadi sasa, maafisa wa Marekani hawajatoa maelezo zaidi kuhusu utambulisho wa dereva huyo au sababu zinazoweza kuwa zimepelekea tukio hilo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha