Wananchi na Waumini wa Bukoba Mjini kutoka makundi na jamii mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuchangia damu, jambo lililoonesha moyo wa ubinadamu, uzalendo na mapenzi kwa wenzao. Zoezi hilo limeelezwa kuwa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji damu kwa dharura, akiwemo mama wajawazito, watoto na waathirika wa ajali.

8 Desemba 2025 - 21:28

Bukoba Mjini | Waumini Wafanya Tukio la Utu kwa Kuchangia Damu Kuokoa Maisha ya Wagonjwa Mahospitalini +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Tukio muhimu la uchangiaji damu lililohusisha Shia Development Organization kwa ushirikiano na JAI limefanyika kwa mafanikio makubwa katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, likiwa na dhamira ya kuokoa maisha ya wagonjwa wanaokabiliwa na upungufu wa damu katika hospitali za eneo hilo.

Waandaaji wa tukio hilo wamesisitiza umuhimu wa jamii kujenga utamaduni wa kujitolea, hasa kwa kuwasaidia watu wasiojiweza na wale waliolazwa hospitalini wanaohitaji damu ili kuendelea kupata tiba. Wameeleza kuwa mafundisho ya Kiislamu kupitia watukufu wa Ahlul-Bayt (a.s) yanahimiza kwa dhati thamani ya utu, huruma na kusaidiana katika kujenga jamii yenye mshikamano.

Wananchi na Waumini wa Bukoba Mjini kutoka makundi na jamii mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuchangia damu, jambo lililoonesha moyo wa ubinadamu, uzalendo na mapenzi kwa wenzao. Zoezi hilo limeelezwa kuwa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji damu kwa dharura, akiwemo mama wajawazito, watoto na waathirika wa ajali.

Shia Development Organization na JAI zimeahidi kuendeleza kampeni kama hii mara kwa mara, ili kusaidia juhudi za sekta ya afya na kuokoa maisha ya watu wengi zaidi katika mkoa na taifa kwa ujumla.

Bukoba Mjini | Waumini Wafanya Tukio la Utu kwa Kuchangia Damu Kuokoa Maisha ya Wagonjwa Mahospitalini +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha