Ziara hiyo imelenga kuhuisha uhusiano wa kitaasisi, kuimarisha umoja, na kuongeza ushirikiano kati ya taasisi za Kiislamu za Shia. Sheikh Jalala ameipongeza Taasisi ya Sayyid Shuhadaa kwa mchango wake mkubwa katika kueneza elimu, maadili mema na huduma za kijamii kwa jamii.

6 Desemba 2025 - 21:13

Sheikh Hemed Jalala Aimarisha Umoja wa Mashia Kupitia Ziara ya Kihistoria Jijini Arusha +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Arusha, Tanzania – Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Maulana Sheikh Hemed Jalala, leo ametembelea Markaz ya Husseiniya ya Imam Ridha (as) iliyopo jijini Arusha, katika mwendelezo wa ziara zake za kitaasisi zenye lengo la kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Mashia nchini.

Markaz hiyo inasimamiwa na Samahat Sheikh Maulid Hussen Sombi chini ya Taasisi ya Sayyid Shuhadaa, ambapo Sheikh Jalala alipokelewa kwa heshima kubwa na viongozi pamoja na waumini wa eneo hilo.

Sheikh Hemed Jalala Aimarisha Umoja wa Mashia Kupitia Ziara ya Kihistoria Jijini Arusha +Picha

Katika ziara hiyo, Sheikh Hemed Jalala alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mahusiano ya kindugu baina ya taasisi za Kiislamu, hususan ndani ya jamii ya Mashia, akibainisha kuwa umoja na mshikamano ni nguzo muhimu katika kulinda maslahi ya Umma na kuendeleza malengo ya kidini na kijamii.

Aidha, Sheikh Jalala aliipongeza Taasisi ya Sayyid Shuhadaa kwa mchango wake mkubwa katika kueneza elimu ya dini, kukuza maadili mema na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa Wananchi wa Arusha na maeneo ya jirani.

Sheikh Hemed Jalala Aimarisha Umoja wa Mashia Kupitia Ziara ya Kihistoria Jijini Arusha +Picha

Kwa upande wake, Samahat Sheikh Maulid Hussen Sombi ameushukuru uongozi wa Jumuiya ya Shia Tanzania pamoja na Taasisi ya Imam Swadiq (a.s) kwa kuendeleza utamaduni wa ziara na kuimarisha mahusiano mema baina ya taasisi za Kiislamu. Amesema ziara hiyo ni chachu ya kuimarisha mshikamano, maelewano na maendeleo ya kijamii na kidini.

Sheikh Hemed Jalala Aimarisha Umoja wa Mashia Kupitia Ziara ya Kihistoria Jijini Arusha +Picha

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kusomwa dua maalum ya kuombea umoja, amani na mshikamano wa Umma wa Kiislamu, huku viongozi wakiahidi kuendeleza ushirikiano kwa maslahi mapana ya jamii.

Sheikh Hemed Jalala Aimarisha Umoja wa Mashia Kupitia Ziara ya Kihistoria Jijini Arusha +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha