Katika nasaha zake kwa wanandoa, Sheikh Jalala amewahimiza kujenga ndoa yenye misingi ya utulivu, mapenzi, heshima, subira, huruma na mawasiliano mema, akisisitiza kushikamana na maadili ya Kiislamu kama nguzo kuu ya ndoa yenye baraka na mafanikio.

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Maulana Sheikh Hemed Jalala, ameungana na waumini pamoja na viongozi wa dini katika kushuhudia hafla ya ndoa ya mtoto wa Sheikh Abuu Ayman iliyofanyika jijini Arusha. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Masheikh mbalimbali, jamaa na wageni waalikwa kutoka maeneo tofauti ya nchi.

Katika nasaha zake kwa wanandoa, Sheikh Jalala amewahimiza kujenga ndoa yenye misingi ya utulivu, mapenzi, heshima, subira, huruma na mawasiliano mema, akisisitiza kushikamana na maadili ya Kiislamu kama nguzo kuu ya ndoa yenye baraka na mafanikio.

Ndoa hiyo ilifungwa rasmi na Samahat Sheikh Maulidi Sombi, na kuhitimishwa kwa mawaidha na dua maalum za kuwaombea wanandoa maisha yenye kheri, amani na maelewano mema.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa dini akiwemo Sheikh Dr. Abdurrazak Amir pamoja na Samahat Sheikh Salman Mgawe, mlezi wa Taasisi ya ABC Center - Jijini Arusha.
Your Comment