Katika taarifa aliyotoa, Abbott pia ametangaza kizuizi cha umiliki wa ardhi ndani ya Texas kwa Baraza la CAIR. Haya yanajiri huku serikali ya shirikisho ya Marekani ikiwa haijawahi kuiweka Ikhwanul Muslimin au CAIR katika orodha ya mashirika ya kigaidi.
Maafisa wa Marekani wametangaza kuwa jioni ya Jumanne wamemkamata mwanaume mmoja baada ya gari lake kugongana na kizuizi cha usalama kilichoko mbele ya lango la kuingilia Ikulu ya White House.