Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa alisema kwamba usalama wa Iran unategemea usalama wa majirani zake na kuongeza:
“Mkataba wa usalama kati ya Iran na Iraq unaandaliwa na utaasainiwa katika safari hii.”
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imemuita balozi wa Uingereza mjini Baghdad kutokana na matamshi yake kuhusu nafasi ya Hashd al-Shaabi katika mfumo wa usalama wa Iraq, na imeonyesha majibu makali juu ya kauli hizo.