2 Oktoba 2025 - 17:54
Amesema kuwa taarifa ya Kundi la G7 kuhusu kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran ni ya kinafiki na yenye upotoshaji.

Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amelaani na kulikemea tamko la Kundi la G7 kuhusu suala la nyuklia la Iran, akilitaja kuwa ni la kinafiki na kupotosha ukweli.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa na kulaani msimamo wa nchi wanachama wa Kundi la 7 (G7) kuhusu kukaribisha hatua isiyo halali na isiyo na msingi ya Marekani na nchi tatu za Ulaya katika kurejesha maazimio ya Baraza la Usalama dhidi ya Iran ambayo yalishafutwa. Amesema hatua hiyo ni sawa na kuunga mkono kitendo cha kukiuka sheria za kimataifa, na akasisitiza kwamba kauli ya G7 kamwe haiwezi kubadilisha uhalisia wa kinyume cha sheria na kutokuwa na msingi kwa hatua hiyo.

Akiashiria uvamizi wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran katikati ya mazungumzo ya kidiplomasia kwa ushirikiano na Marekani, na pia shambulizi la moja kwa moja la Marekani dhidi ya mitambo ya nyuklia ya Iran, msemaji huyo alisema kuwa madai ya G7 kwamba Marekani na nchi tatu za Ulaya mara kadhaa “ziliwasilisha suluhu za kidiplomasia kwa nia njema” ni uongo mtupu na kupindisha ukweli. Alisisitiza kuwa Marekani ndiyo chanzo na sababu kuu ya hali ya sasa kwa sababu ya kujiondoa kwake kinyume cha sheria na kwa upande mmoja kutoka makubaliano ya nyuklia (JCPOA) mnamo mwaka 2018, pamoja na ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria za kimataifa na kuweka vikwazo dhidi ya Iran. Vilevile, nchi tatu za Ulaya, kwa kufuata Marekani na kushindwa kutekeleza wajibu wao, sambamba na kuunga mkono Marekani na Israel katika uvamizi dhidi ya mitambo ya nyuklia yenye matumizi ya amani ya Iran, wamefanya “kutotekeleza kwa kiwango kikubwa” wajibu wao chini ya JCPOA na kwa dhahiri kupuuza jitihada zote za Iran za kidiplomasia.

Aidha, msemaji huyo aliongeza kuwa kutojali kwa wanachama wa G7 kuhusu ghala la silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni unaoendesha mauaji ya kimbari, kunadhihirisha unafiki wao katika suala la kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia. Amesisitiza kwamba nchi hizo saba, kwa sababu ya mienendo yao ya kinafiki na isiyo na uwajibikaji kuhusu utawala wa sheria, amani na usalama wa kimataifa, hazina uhalali wa kimaadili wowote wa kuhubiri mataifa mengine.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha