Mkono
-
Ismail Baghaei – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran:
Amesema kuwa taarifa ya Kundi la G7 kuhusu kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran ni ya kinafiki na yenye upotoshaji.
Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amelaani na kulikemea tamko la Kundi la G7 kuhusu suala la nyuklia la Iran, akilitaja kuwa ni la kinafiki na kupotosha ukweli.
-
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan:
"Kuitambua tu Palestina hakutoshi - Hatua za vitendo pia ni muhimu"
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan amesisitiza: "Nchi ambazo hapo awali zilikuwa kimya au hata ziliunga mkono utawala haramu wa Kizayuni (Israel), leo hii zinajifanya kupinga ukatili wa utawala huo na zinaanza kuutambua rasmi uhuru wa Palestina. Ingawa hii inaonekana kama hatua chanya kwa mtazamo wa nje, haitoshi kama haitafuatiwa na hatua madhubuti."
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Lebanon katika mahojiano na ABNA:
"Baada ya kuondolewa kwa silaha za Hizbullah, hakuna dhamana ya kulinda Lebanon dhidi ya adui msaliti"
Adnan Mansour: Je, viongozi rasmi wa Lebanon wanaweza kusimama dhidi ya Marekani na kulinda maslahi ya Lebanon na hatari za kuondolewa kwa silaha? Nani atakayebaki Lebanon kupambana na uvamizi wa Israel? Je, jeshi la Lebanon linaweza kukabiliana na uvamizi peke yake? Kamwe.
-
Utekelezaji wa Majaribio wa Mpango wa "Shule Huru" katika Hawza ya Qom
Naibu Meneja wa Hawza ya Qom ametangaza kupitishwa kwa mpango wa “Shule Huru” na kuanza kutekelezwa kwa majaribio.