Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- TUNGUU, ZANZIBAR – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 06, 2026, amefanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wakuu wa wizara na majeshi ikiwa ni pamoja na:
1_Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho
2_Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka
3_Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Dkt. Faraji Mnyepe
4_Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda
5_Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele.

Mazungumzo hayo yamezingatia masuala mbalimbali ya usalama, ulinzi wa taifa, na maendeleo ya majeshi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya majeshi na wananchi katika kuhakikisha amani na utulivu wa taifa.
Rais Samia pia alisisitiza kuimarisha mafunzo, usalama wa rasilimali, na ufanisi wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Your Comment