7 Agosti 2025 - 13:13
Sheikh Dr. Alhad Musa Salum Akabidhiwa Tuzo ya Uongozi wa Mfano na JMAT Mkoa wa Dar -es- Salaam

Tukio hilo lilifanyika katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa JMAT kwa Muhula wa Kwanza wa Mwaka 2025, ambapo viongozi mbalimbali wa kidini na kijamii walihudhuria.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Agosti 2025 - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Christosiler Kalata, amemkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania - JMAT-TAIFA- , Sheikh Dr. Alhad Musa Salum, tuzo ya Uongozi wa Mfano, ikiwa ni kutambua mchango wake katika kukuza umoja, mshikamano na maadili ya uongozi bora nchini.

Tukio hilo lilifanyika katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa JMAT kwa Muhula wa Kwanza wa Mwaka 2025, ambapo viongozi mbalimbali wa kidini na kijamii walihudhuria.

Kwa mujibu wa viongozi wa JMAT Mkoa, tuzo hiyo imetolewa kwa niaba ya uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kama ishara ya kuthamini juhudi za Sheikh Dr. Alhad Musa Salum katika kujenga jamii yenye mshikamano, amani na maelewano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini.

Katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo, Sheikh Alhad Musa alieleza kuwa heshima hiyo si yake binafsi bali ni kwa niaba ya viongozi wote wanaojituma katika kuimarisha misingi ya maelewano ya kitaifa. Alisisitiza haja ya kuendeleza mazungumzo ya kidini na kushirikiana katika masuala ya kijamii na maendeleo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha