Mkutano huu ni katika muktadha wa kudumisha Amani na Utulivu wa Taifa letu la Tanzania na kulitakia Kheri na Baraka Taifa hili kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Wananchi.
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania tutasimama na Serikali Daima katika kulinda na kudumisha Amani na Maridhiano ya nchi yetu kwa ajili ya Ustawi wa nchi yetu.
Lengo kuu la Matembezi haya: Kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu. Kauli Mbiu: “Uchaguzi wa AMANI Ndio Msingi wa UTULIVU Wetu.”