Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Arusha, Tanzania – Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), Askofu Dkt. Gabriel Ole Maasa, ameshiriki katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Ushiriki wa Katibu Mkuu huyu katika kikao hicho umeonesha dhamira ya dhati ya JMAT-TAIFA katika kuimarisha mashirikiano na taasisi za kitaifa na kimataifa, hususan katika kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali za kijamii.
Sehemu ya Sifa za Uongozi Wake na Majukumu Yake
Miongoni mwa sifa zinazomtambulisha Askofu Dkt. Maasa - hususan Jijini Arusha - ni jitihada zake za kuhakikisha kuwa mahitaji ya msingi ya binadamu kama maji safi, huduma za afya na dawa yanapatikana kwa urahisi kwa wananchi wa maeneo yenye uhitaji.
Ushirikiano na Mashirika ya Umma na Kimataifa
Kupitia JMAT-TAIFA, Katibu Mkuu ameweza kuikutanisha jumuiya na mashirika kadhaa ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo “ALL FOR HIS GLORY” pamoja na mengineyo. Mashirikiano haya yamewezesha utekelezaji wa miradi muhimu ya kijamii kama vile:
- Uchimbaji wa visima katika vijiji vyenye uhitaji.
- Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya.
- Uhakika wa upatikanaji wa dawa katika maeneo ya vijijini.
Wito na Baraka kwa Taifa
Kwa kujitoa kwake bila ubinafsi, Askofu Dkt. Maasa ameendelea kuacha alama ya kumbukumbu isiyofutika katika maisha ya jamii. Juhudi hizi ni kielelezo cha dhati cha falsafa ya JMAT-TAIFA – kuendeleza amani, mshikamano na ustawi wa wananchi wote.
Mungu Ibariki Tanzania – Tanzania Yetu, Amani Kwanza.
Your Comment