Maridhiano
-
Askofu Dkt.Gabriel O.Maasa Aiwakilisha Vyema JMAT-TAIFA -Katika Ushirikiano wa Kijamii na Taasisi za Umma- Katika Kikao Kazi cha Kitaifa Jijini Arusha
Askofu Dkt. Maasa ameendelea kuacha alama ya kumbukumbu isiyofutika katika maisha ya jamii. Juhudi zake ni kielelezo cha dhati cha Falsafa ya JMAT-TAIFA - kuendeleza Maridhiano, Amani, Mshikamano na Ustawi wa Wananchi wote.
-
JMAT TAIFA:
Mdahalo wa Viongozi wa Dini na Siasa: Wito wa Kudumisha Amani na Demokrasia Safi kuelekea Uchaguzi Mkuu
Sheikh Dkt. Al-Hadi Mussa Salum: "Amani na Utulivu nchini ni msingi wa maendeleo ya Taifa na Ustawi wa kila Mtanzania".
-
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania:
Viongozi wa Kitaifa wa JMAT-TAIFA Wajadili Ajenda za Amani na Maridhiano Jijini Arusha
Askofu Profesa Rejoice Ndalima: "Inafaa na inapendeza kwa viongozi wa kijamii na kidini kuungana ili kupunguza migawanyiko na kuondoa maneno ya chuki miongoni mwa Wananchi".
-
Maneno Muhimu na ya Hekima ya Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum - kuhusu: Wanaoitwa Mitume na Manabii Tanzania, Udugu wa Watanzania, na Amani ya Tanzania
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania tutasimama na Serikali Daima katika kulinda na kudumisha Amani na Maridhiano ya nchi yetu kwa ajili ya Ustawi wa nchi yetu.
-
Dkt. Al-Had Mussa Salum - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) Azungumzia Mambo Matatu Muhimu kwa Mustakbali wa Taifa
JMAT imepanga kuendesha matembezi ya amani kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Lengo ni kuleta Watanzania pamoja na kuhamasisha Amani na Maridhiano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.
-
Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga
Ni katika Kongamano la Qur'an Tukufu lililofanyiks Jijini Tanga. Tukio hilo liliimarisha misingi ya Amani, Mshikamano, Maridhiano, na Ushirikiano kati ya Watanzania, likiwa ni Jukwaa la kuendeleza Mafundisho ya Qur’an Tukufu yanayohimiza Utulivu na Maelewano ya Kijamii.
-
JMAT Yatoa Wito kwa Viongozi wa Dini Nchini Kenya wa Kushirikiana Katika Kuwaongoza Wananchi wao ili Kuheshimiana na Kutunza Mahusiano ya Amani
Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum: "Wakenya ni ndugu wa Watanzania, na mbali na uhusiano wa kijamii, ni ndugu wa damu. Tunatambua kuwa mizozo hii inahusu zaidi vijana wa Kenya, lakini ni muhimu kuwakumbusha kuwa heshima ni nguzo muhimu katika mahusiano ya mataifa. Tunaamini Kenya ina Viongozi wa Dini na Serikali wanaoweza kusaidia katika hili."
-
Ufafanuzi wa Kina na Maridhawa Juu ya Suala la Unabii Baina ya Waislamu na Wakristo
Sheikh Dk.Alhad Mussa Salum: "Wakristo wanaposema, au tunaposikia ikisemwa, au anapoitwa mtu kuwa ni Nabii au Nabii Mkuu, anaitwa hivyo kwa Istilahi ipi?! Hili ndio swali la msingi kujiuliza?. Anaitwa hivyo kwa Istilahi yetu sisi Waislamu au kwa istilahi yao hao ndugu zetu Wakristo?!. Kwa sababu katika suala la UNABII kila watu wana Istilahi zao".