29 Mei 2025 - 22:58
Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA 
Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga

Ni katika Kongamano la Qur'an Tukufu lililofanyiks Jijini Tanga. Tukio hilo liliimarisha misingi ya Amani, Mshikamano, Maridhiano, na Ushirikiano kati ya Watanzania, likiwa ni Jukwaa la kuendeleza Mafundisho ya Qur’an Tukufu yanayohimiza Utulivu na Maelewano ya Kijamii.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tanga - Tanzania: Katika Matukio ambayo sio rahisi kuyasahau ni pamoja na tukio la Kongamano kubwa la Qur'an Tukufu lililofanyika tarehe 24 Mei, 2025, likiwatanisha maelfu ya Washiriki katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Jijini Tanga. 

Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA 
Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga

Katika Kongamano hilo, Firdaus TV ilifanya mahojiano maalum na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimam wa Tanzania (JMAT-TAIFA), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Wasomaji Bingwa wa Qur’an Tukufu kwa Njia ya Tajweed kutoka Iran na Tanzania, pamoja na Viongozi wa Serikali, Taasisi za Kidini, na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za nchi ya Tanzania.

Tukio hilo liliimarisha misingi ya Amani, Mshikamano, Maridhiano, na Ushirikiano kati ya Watanzania, likiwa ni Jukwaa la kuendeleza Mafundisho ya Qur’an Tukufu yanayohimiza Utulivu na Maelewano ya Kijamii.

Kupitia Firdaus TV - Katika ujumbe wake, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum alisisitiza kwamba:

"Mwanadamu asili yake ni Amani. Tuitunze Amani yetu kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu."

Akirejea Aya ya Qur’an Tukufu (Surat Yunus: Aya ya 25):

Na Mwenyezi Mungu anawaita kwenye Nyumba ya Amani…”

Sheikh Dkt.Alhad alieleza kuwa wito huu wa Kiungu unapaswa kuwa msingi wa maisha yetu ya kila siku kama Taifa lenye malengo ya kudumu ya maendeleo na mshikamano.

Kwa ujumla, Kongamano hili liliacha athari chanya na ya kudumu katika nyoyo za Washiriki, likiwa ni alama ya udugu na umoja chini ya mwamvuli wa Maandiko Matakatifu.

Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA 
Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha