Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi, Uwajibikaji na Mahusiano ya JMAT-TAIFA, Mhe. Bi Leila Bhanj, ameshiriki katika kikao kazi maalumu kilichokutanisha mihimili ya nchi upande wa sheria.
Kikao hicho kiliongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Masaju, kwa kushirikiana na Jaji Kiongozi, Mhe. Siyani, pamoja na Jaji wa Rufaa Tanzania, Mhe. Mwarija.
Ushiriki wa Bi.Leila katika kikao hicho umetajwa kuwa ni uwakilishi mkubwa wa JMAT-TAIFA, ambapo mijadala ilihusu masuala ya utawala bora na uwajibikaji katika mfumo wa sheria.
Kikao hicho kimefanyika Dodoma, Mji Mkuu wa Tanzania.
Habari hii imetolewa kwa hisani kubwa ya:
Abdillah Fundi – Naibu Mkurugenzi Utalii na Utamaduni.
Your Comment