Mkutano huu ni katika muktadha wa kudumisha Amani na Utulivu wa Taifa letu la Tanzania na kulitakia Kheri na Baraka Taifa hili kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Wananchi.
JMAT imepanga kuendesha matembezi ya amani kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania. Lengo ni kuleta Watanzania pamoja na kuhamasisha Amani na Maridhiano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.
Lengo kuu la Matembezi haya: Kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu. Kauli Mbiu: “Uchaguzi wa AMANI Ndio Msingi wa UTULIVU Wetu.”