15 Novemba 2025 - 22:01
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini

Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya: a) Vifaa tiba, b) Dawa, c) Na maboresho ya miundombinu ya afya.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Rufaa Dodoma; atoa maagizo mazito kuboresha huduma kwa wajawazito na upatikanaji wa dawa. Ufuatao ni Muhtasari wa Ziara ya Mheshimiwa Waziri.

Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini

1. Ziara ya kushtukiza

a) Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza leo 15 Novemba 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

b) Lengo: kukagua hali ya utoaji huduma na kuzungumza na wananchi waliokuwa wakipata matibabu.

2. Maagizo kuhusu huduma kwa wajawazito

Dkt. Mwigulu ameziagiza hospitali zote nchini:

a) Kuhudumia wajawazito kwa haraka na kipaumbele ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

b) Kuwa na vifaa vya dharura katika wodi za wazazi, ikiwemo ndoo na mabalaza/beseni, ili kuwasaidia wajawazito wasiokuwa na vifaa hivyo.

Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini

3. Upatikanaji wa dawa nchini

Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Afya, MSD na hospitali zote kwamba:

a) Lazima kuwepo upatikanaji wa dawa kulingana na mahitaji halisi ya kila eneo.

b) Ameonya kuwa si jambo linalokubalika mgonjwa kufanyiwa vipimo hospitalini kisha kuambiwa akanunue dawa nje.

c) Hospitali za serikali zinapaswa kuwa na dawa za kutosha kwa wakati wote.

4. Uboreshaji wa huduma za afya

Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya:

  • a) Vifaa tiba,
  • b) Dawa,
  • c) Na maboresho ya miundombinu ya afya.

    Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini

Wananchi waliokutana na Waziri Mkuu wamethibitisha kuwa huduma katika hospitali hiyo zinatolewa vizuri.

5. Udhibiti wa mfumo wa malipo

a) Amesisitiza hospitali zote kutumia mifumo rasmi ya malipo ya Serikali.

b) Amekemea baadhi ya vituo vinavyotoa huduma na kukusanya fedha kupitia njia zisizo rasmi.

c) Mfumo sahihi wa malipo utaiwezesha Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha