kiswahili
-
"Hezbollah ya Lebanon imetoa pole kwa Kiongozi wa Mapinduzi na Taifa la Iran kufuatia tukio la Mlipuko wa Bandar Abbas"
Baada ya tukio la kusikitisha katika Bandari ya Shahid Rajaei Bandar Abbas lililosababisha mashahidi na majeruhi kadhaa, Hezbollah ya Lebanon imetoa taarifa ya kuonesha mshikamano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-e-Salam, Tanzania, katika ziara muhimu Zanzibar - Tanzania + Picha
"Ni muhimu kwa Wanafunzi kuzingatia elimu na maarifa ya Qur'an Tukufu, na kuwaasa katika kuzidisha juhudi zao kwenye suala muhimu la kusoma na kuhifadhi Qur'an Tukufu, na kuiweka Qur'an Tukufu mbele ya Maisha yao ya kila siku".
-
Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) | Jua la Elimu na Uchaji Mungu Limezimwa
Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) haikuwa tu kumpoteza kiongozi wa kiroho, bali ilikuwa ni jaribio la kuangamiza nuru ya elimu na mwongozo wa Ahlul Bayt(a.s). Hata hivyo, athari ya mafundisho yake bado inaishi hadi leo kupitia Maktaba ya Ja’fariyya, ambayo ni msingi wa Madhehebu ya Shia Ithna ‘Ashari.
-
Mkutano wa Mufti wa Burundi na Mwakilishi wa Al-Mustafa (s) Nchini Tanzania + Picha
Mufti wa Burundi akutana na kuzungumza na Hojjatul Islam wal-Muslimin, Dr.Ali Taqavi Katika Ofisi ya Al-Mustafa (s) Dar -es- Salaam - Tanzania.
-
Morocco; Imeshuhudia Mikusanyiko 105 ya Kuunga Mkono Palestina
Al Jazeera Qatar imeripoti kuwa, (mikusanyiko) maandamano 105 yalifanyika katika miji 58 ya Morocco katika kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Gaza.
-
Al_Itrah Foundation, Dar-es-salaam - Tanzania yampa zawadi ya Tafsiri ya Kiswahili ya Qur'an Tukufu Mwenyekiti wa JMAT - TAIFA Sh.Dr Alhad Mussa Salum
"Kitabu Hicho Hakina Shaka ndani yake, ni Muongozo kwa Wacha Mungu".
-
Historia | Tarehe 8 Shawwal 1345 Hijria, Mawahhabi walibomoa na kuyanajisi Makaburi ya Ahlu Bayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Mji wa Madina
Historia inaonyesha kuwa, katika tukio hilo la kusikitisha, lililotokea tarehe 8 Mfunguo Mosi Shawwal 1345 Hijria (1925 Miladia) Mawahabi wa Saudi Arabia walibomoa makaburi ya Ahlul-Bayt -a.s- wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambayo yanapatikana katika ardhi ya Baqi’i, katika Mji Mtakatifu wa Madina.
-
UNICEF: Maisha ya watoto milioni moja huko Gaza yako hatarini
Wakati huo huo hujuma zikiendelea na ugavi wa misaada kwa Gaza ukikatizwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto lilionya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hili na kutangaza kwamba maisha ya watoto wapatao milioni moja katika ukanda huu yako chini ya hatari na tishio kubwa.
-
Ndege nyingine isiyo na rubani ya Marekani imetunguliwa ndani anga la Yemen
Ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani imdunguliwa katika mMkoa wa Marib.
-
Siku ya Quds Duniani:
Kongamano la Siku ya Quds Duniani lilifanyika Jijini Tanga, Tanzania
Kuna umuhimu Mkubwa kwa Waislamu na Watu wote huru na wapenda Haki Duniani, kuzidi kusimama pamoja na wadhulumiwa wa Palestina na kutetea Haki za watu wote wanyonge popote pale walipo Duniani. Watu mbalimbali kutoka Jiji la Tanga walihudhuria katika Mkusanyiko huu wa kuhuisha Siku ya Kimataifa ya Quds, wakiwemo Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kidini na Madhehebu mbalimbali.
-
Ni Ipi Hukumu ya Mwanamke Kufunga Bila ya Idhini ya Mumewe?
Mume na Mke wako huru kutekeleza majukumu yao ya Faradhi ya Shariah, na kitendo cha wote wawili kiko chini ya idhini ya mwingine. Na funga (Saumu) ya Wajibu pia iko hivyo.
-
Mwaliko (Wito) wa Ayatollah Ramadhani kwa watu wa Gilan Kushiriki Katika Maandamano ya Siku ya Quds ya 2025
Ayatollah "Reza Ramezani", Mwakilishi wa Wananchi wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika Mkesha wa Siku ya Quds Duniani, amewaalika na kuwahimiza watu kushiriki katika Maandamano ya Siku hii.
-
Gwaride la Boti 3,000 za Kijeshi za Iran litafanyika kuwaunga Mkono Wananchi wa Palestina
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limetangaza Gwaride la Boti za Kijeshi 3,000 na uhamasishaji wa Wananchi kwa ajili ya kuwaunga mkono Wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Njia ya Dhambi Huanza na Dakika ya Uzembe
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote tupate taufiki ya kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani wao ndio Njia iliyonyooka, na atakayeshikamana nao wao na Qur'an Tukufu, huyo ataepukana na upotevu, kwa sababu wao ndio sehemu ya Kizito cha pili baada ya Qur'an Tukufu, na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ametuusia katika Hadithi Sahih na Mutawatiri ya Thaqalayni, kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na Quran Tukufu ili tuje kupotea baada yake.
-
Thamani ya Usiku wa Lailatul - Qadri:
Miezi Elfu Moja (1,000) ni sawa na: Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika Usiku huu wa Cheo (Lailatul-Qadri) utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika Usiku huu na ukose kufanya ibada, utapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.
-
Mashahidi 38 wa Kipalestina; Uovu mpya wa utawala wa Kizayuni huko Gaza
Katika muendelezo wa mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni umeua idadi nyingine ya Wapalestina.
-
Tutajitahidi kufanya thamani yetu kuwa bora zaidi na ya juu zaidi kuliko ilivyo kwa sasa katika mzunguko mpya wa nyakati
Akisema kwamba Nowruz na na Nyusiku za Lailat al-Qadr ni miale miwili ya nuru moja na madhihirisho mawili ya ukweli uleule (ulio sawa), Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tunakesha katika usiku huu ili kuwa Wanadamu wapya kwa kuzisafisha nafsi zetu na kufikia hatima (makadirio) yetu katika siku mpya, lakini hatima (makadirio) yetu na nchi yetu si mahali hapa tuliposimama; Uthamani wetu ni wa juu kuliko hali yetu ya sasa.
-
Takriban Maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa Shahidi katika Mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza
Takriban maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
-
Radiamali ya Seneta RajA Nasser kwa mauaji ya Mwanazuoni wa Pakistan
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amelaani mauaji ya Mufti Munir Shakir, Mwanazuoni wa Kisunni wa Pakistan, na kuyataja kuwa ni hasara isiyoweza kufidiwa.
-
Sayyid Abdul Malik al-Houthi: Meli za Marekani ni marufuku pia kupita Bahari Nyekundu
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema: Tutajibu ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano. Kuanzia sasa, sambamba na kupiga marufuku kupita kwa meli za Israeli katika Bahari Nyekundu, kupita kwa meli za Marekani pia ni marufuku.
-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dokta Abubakar Zuber Ali Mbwana:
"Maendeleo sio ugomvi, bali ni kufanya mambo yanayoonekana na yanayompendeza Mwenyezi Mungu"
Msikiti ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ni Kituo cha kiroho, kijamii na kiutamaduni, na vile vile ni nyumba makhsusi kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali ndani yake.
-
Uwepo wa magaidi kutoka nchi 20 katika Serikali ya Syria | Serikali ya mpito au Mradi wa Kikoloni!
Vyanzo vyenye maarifa na utambuzi, vimetoa taarifa juu ya kuundwa kwa muundo mpya wa usalama katika utawala wa Kigaidi wa al-Jolani.
-
Kuwatukana wakubwa wa kidini; Asili, motisha na haiba, shakhsia ya upuuzi ya wadhalilishaji
Kuwatukana viongozi wakubwa wa kidini, daima imekuwa moja ya masuala nyeti na changamoto katika jamii za kidini. Jambo hili sio tu linaumiza hisia za waumini, lakini pia linaonyesha upungufu wa maadili na tabia mbaya ya wadhalilishaji.