Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA-; Sheikh Siraji Salanga, katika la Darsa lake ndani ya Masiku Matukufu ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, katika Masjid Al-Zahraa (s.a), Arusha - Tanzania, amewalingania Waumini kushikamana na Matendo Mema na Mazuri na kuzitafuta daima Radhi za Mwenyezi Mungu (s.w.t). Pia Muislamu anatakiwa siku zote kujiepusha na tabia ya uzembe na kupuuzia kufanya mambo ya kheri, na akaongeza kusema:
"Njia ya dhambi huanza na ile dakika ya uzembe. Uzembe wako utasababisha utende dhambi zaidi, uzembe wako utapekelea uweze kujiangamiza zaidi, hali ya kuwa njia nzuri za kukuokoa na kukutoa huko uliko, zipo nyingi, miongoni mwa njia hizo nzuri, ni kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s), wao ndio Njia iliyo nyooka.
Tunapo Swali kila Siku Swala Tano, huwa tunasoma katika Swala zetu Surat Al_Fa'tiha, na tunapofika katika Aya ya 6 huwa tunasoma Aya hiyo tukisema:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾
"Tuongoze katika Njia iliyonyooka" (6).
Katika Aya hii Tukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) atuongoze katika Njia iliyonyooka.
Imam Jaafar Sadiq (a.s) katika kuitafsiri Aya hii anasema:
"إهدنا الصراط المستقيم: الطريق هو معرفة الإمام".
"Njia iliyonyooka, ni Kumtambua (Kumfahamu) Imam".
Pia imepokewa kutoka kwake (sehemu nyingine) kuhusiana na:
(إهدنا الصراط المستقيم).
Akisema:
"والله نحن الصراط المستقيم:
"Wallah Sisi (Ahlul-Bayt) ndio Njia iliyonyooka".
Rerea:
تفسير نور الثقلين، ج 1، ص (20 و 21).
Tafsir Nuru Al-Thaqalayni: Juzuu ya 1: Ukurasa wa 20.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote tupate taufiki ya kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani wao ndio Njia iliyonyooka, na atakayeshikamana nao wao na Qur'an Tukufu, huyo ataepukana na upotevu, kwa sababu wao ndio sehemu ya Kizito cha pili baada ya Qur'an Tukufu, na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ametuusia katika Hadithi Sahih na Mutawatiri ya Thaqalayni, kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na Quran Tukufu ili tuje kupotea baada yake, anasema:
(إنّي تاركٌ فيكم الثقلين ما إن تَمَسَّكتم بهما لن تضلّوا بعدي: كتاب الله وعترتي أهلَ بيتي، لن يفترقا حتى يردا عليّ الحوضَ).
“Hakika mimi nimekuachieni vizito viwili, ambavyo ikiwa mtashikamana navyo, basi hamtapotea baada yangu, (navyo ni) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah wangu Ahlul-Bayt wangu (Familiya yangu), (vizito hivi viwili) havitokuja kutofautiana kamwe mpaka vitakaponirudia katika Haudhi”.
-
Rejea ya Kisunni ya Hadithi hii:
1- (Al-Nasa’i, al-Sunan al-Kubra, 1411 H, Juzuu ya 5, Ukurasa wa 45).
Rejea ya Kishia ya Hadithi hii:
2- Al-Kulaini, Al-Kafi, Juzuu ya 1, Ukurasa wa 294).
Your Comment